Mwongozo

Jinsi ya kugawa video ndefu kwa status ya WhatsApp

Status ya WhatsApp inakubali video fupi tu, hivyo video ndefu inakatika. PigaTools inaigawa kuwa vipande vya sekunde 30 au 60 unavyopost kimoja baada ya kingine - bure, na video haitoki kwenye simu yako.

  1. 1

    Fungua zana ya status

    Bonyeza kitufe hapa chini, au fungua PigaTools uchague Status ya WhatsApp.

  2. 2

    Chagua video yako

    Ichague kwenye gallery yako. Video za hadi dakika 15 zinakubali.

  3. 3

    Chagua urefu wa vipande

    Sekunde 30 zinafanya kazi kwenye WhatsApp yoyote; WhatsApp mpya inakubali pia sekunde 60. Chagua "Wima 9:16" ili video ijaze skrini nzima.

  4. 4

    Tengeneza na hifadhi vipande

    Bonyeza "Tengeneza vipande vya status". Vikiwa tayari, save kila kipande - vinaenda kwenye Downloads au gallery yako.

  5. 5

    Viposti kwa mpangilio

    Kwenye WhatsApp, weka Kipande 1 kwenye status yako, kisha Kipande 2 na kuendelea, ili watu wako wavitazame kwa mpangilio.

Fungua zana ya status Bure · inafanya kazi kwenye simu yako · faili lako halitumwi popote

Vidokezo

  • Vipande vinatengenezwa kwenye simu yako, hivyo video ndefu inaweza kuchukua dakika moja au mbili - usifunge ukurasa.
  • Vipande vya bure ni 720p - vidogo na vinapostika haraka. Vipande vya HD 1080p ni vya Pro.

Maswali

Je, ni bure?

Ndiyo. Kugawa video kwa status ni bure bila kikomo, na hakuna watermark.

Je, video yangu inatumwa mtandaoni?

Hapana. Inakatwa ndani ya browser yako, kwenye simu au kompyuta yako mwenyewe.

Miongozo mingine